Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yohana 19:31-34

Yohana 19:31-34 NENO

Ilikuwa siku ya Maandalio ya Pasaka, na siku iliyofuata ingekuwa Sabato maalum. Kwa kuwa viongozi wa Wayahudi hawakutaka miili ibaki msalabani siku ya Sabato, wakamwomba Pilato aamuru miguu ya wale waliosulubiwa ivunjwe, na miili iondolewe kwenye misalaba. Kwa hiyo askari wakaenda wakavunja miguu ya mtu wa kwanza aliyesulubiwa pamoja na Isa, na ya yule mwingine pia. Lakini walipomkaribia Isa, wakaona ya kuwa amekwisha kufa, hivyo hawakuvunja miguu yake. Badala yake mmoja wa wale askari akamchoma mkuki ubavuni, na mara pakatoka damu na maji.