Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hagai Utangulizi

Utangulizi
Hagai ni moja ya vitabu vitatu kati ya vitabu vya Manabii vilivyoandikwa baada ya Wayahudi kurudi nyumbani kutoka uhamishoni Babeli. Baada ya Mfalme Dario kutoa amri ya kuwaruhusu Wayahudi kurudi Yerusalemu kutoka uhamishoni, Hagai na Zekaria waliwatia moyo watu hao kulijenga upya Hekalu la Bwana.
Kundi la kwanza la Wayahudi liliporudi Yerusalemu liliweka msingi wa Hekalu jipya kwa furaha na matumaini makubwa. Hata hivyo, Wasamaria na majirani wengine walipinga ujenzi huo kwa nguvu nyingi na kuwakatisha tamaa wafanyakazi, na kusababisha ujenzi huo usimame. Watu wakageukia ujenzi wa nyumba zao wenyewe. Nabii Hagai aliwahimiza watu kwamba ulikuwa wakati wa kuanza kujenga upya nyumba ya Mwenyezi Mungu.
Mwandishi
Hagai.
Kusudi
Kujenga upya Hekalu la Mwenyezi Mungu.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
Mnamo 520 K.K.
Wahusika Wakuu
Hagai, Zerubabeli, Yoshua.
Wazo Kuu
Hagai aliwaambia watu kwamba utukufu wa Hekalu walilokuwa wanajenga ungekuwa mkubwa kuliko ule wa Hekalu lililotangulia, ingawaje halingekuwa imara kama la kwanza. Hili Hekalu lingekuwa bora zaidi kwa sababu Mwenyezi Mungu angelijaza utukufu wake ndani yake.
Mambo Muhimu
Kuwaita watu kujenga upya Hekalu huko Yerusalemu lililokuwa limebomolewa, na ahadi ya Mwenyezi Mungu ya kuwabariki kama wangemtii.
Yaliyomo
Wito wa kujenga Hekalu (1:1-15)
Matumaini ya Hekalu jipya, na baraka zilizoahidiwa (2:1-23).

Iliyochaguliwa sasa

Hagai Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia