Hagai 1:12-15
Hagai 1:12-15 NENO
Kisha Zerubabeli mwana wa Shealtieli, Yoshua kuhani mkuu mwana wa Yehosadaki, pamoja na mabaki yote ya watu wakaitii sauti ya Mwenyezi Mungu, Mungu wao, pamoja na ujumbe wa nabii Hagai, kwa sababu alikuwa ametumwa na Mwenyezi Mungu, Mungu wao. Watu walimwogopa Mwenyezi Mungu. Kisha Hagai, mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akawapa watu ujumbe huu wa Mwenyezi Mungu: “Mimi niko pamoja nanyi,” asema Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akachochea roho ya Zerubabeli mwana wa Shealtieli, mtawala wa Yuda, na roho ya kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki, pamoja na roho za mabaki yote ya watu. Walikuja, wakaanza kufanya kazi katika nyumba ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wao, siku ya ishirini na nne ya mwezi wa sita, katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario.