Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 40:16-23

Mwanzo 40:16-23 NENO

Yule mwokaji mkuu alipoona kuwa Yusufu amefasiri vizuri, akamwambia Yusufu, “Mimi pia niliota ndoto. Kichwani mwangu kulikuwa vikapu vitatu vya mikate. Katika kikapu cha juu kulikuwa na aina zote za vyakula vilivyookwa kwa ajili ya Farao, lakini ndege walikuwa wakivila kutoka kikapu nilichobeba kichwani.” Yusufu akamwambia, “Hii ndiyo maana yake: Vikapu vitatu ni siku tatu. Baada ya siku tatu, Farao atakata kichwa chako na kukutundika juu ya mti. Nao ndege watakula nyama ya mwili wako.” Siku ya tatu ilikuwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Farao, naye akawaandalia maafisa wake wote karamu. Akawatoa gerezani mnyweshaji mkuu na mwokaji mkuu, akawaweka mbele ya maafisa wake. Ndipo akamrudisha mnyweshaji mkuu kwenye nafasi yake, ili aweke kikombe mkononi mwa Farao tena. Lakini akamwangika yule mwokaji mkuu, kama Yusufu alivyowafasiria. Lakini mnyweshaji mkuu hakumkumbuka Yusufu, bali alimsahau.