Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 37:5-9

Mwanzo 37:5-9 NEN

Yosefu akaota ndoto, naye alipowaeleza ndugu zake, wakamchukia zaidi. Akawaambia, “Sikilizeni ndoto niliyoota: Tulikuwa tukifunga miganda ya nafaka shambani, ghafula mganda wangu ukasimama wima, wakati miganda yenu ikiuzunguka na kuuinamia.” Ndugu zake wakamwambia, “Wewe unakusudia kututawala? Hivi kweli wewe utatutawala sisi?” Wakaongeza kumchukia zaidi kwa sababu ya ndoto yake pamoja na yale aliyowaambia. Kisha akaota ndoto nyingine, akawaambia ndugu zake akisema, “Sikilizeni, nimeota ndoto nyingine, wakati huu jua, mwezi na nyota kumi na moja zilikuwa zinanisujudia.”