Mwanzo 19:27-29
Mwanzo 19:27-29 NENO
Asubuhi na mapema siku iliyofuata, Abrahamu akaamka na kurudi mahali pale aliposimama mbele za BWANA. Akatazama upande wa Sodoma na Gomora, kuelekea nchi yote ya tambarare, akaona moshi mzito ukipanda kutoka nchi, kama moshi unaotoka katika tanuru. Kwa hiyo Mungu alipoiangamiza miji ya tambarare, alimkumbuka Abrahamu, akamtoa Lutu kutoka lile janga lililoharibu miji ile ambamo Lutu alikuwa ameishi.