Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 15:13-16

Mwanzo 15:13-16 NEN

Kisha BWANA akamwambia, “Ujue hakika kwamba wazao wako watakuwa wageni kwenye nchi ambayo si yao, nao watafanywa watumwa na kuteswa kwa miaka mia nne. Lakini nitaliadhibu taifa lile watakalolitumikia kama watumwa, na baadaye watatoka huko na mali nyingi. Wewe, hata hivyo utakwenda kwa baba zako kwa amani na kuzikwa katika uzee mwema. Katika kizazi cha nne wazao wako watarudi hapa, kwa maana dhambi ya Waamori bado haijafikia kipimo kilichojaa.”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mwanzo 15:13-16