Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 15:1-6

Mwanzo 15:1-6 NEN

Baada ya jambo hili, neno la BWANA likamjia Abramu katika maono: “Usiogope, Abramu. Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana.” Lakini Abramu akasema, “Ee BWANA Mwenyezi, utanipa nini na mimi sina hata mtoto na atakayerithi nyumba yangu ni huyu Eliezeri Mdameski?” Abramu akasema, “Hukunipa watoto, hivyo mtumishi katika nyumba yangu ndiye atakuwa mrithi wangu.” Ndipo neno la BWANA lilipomjia: “Mtu huyu hatakuwa mrithi wako, bali mwana atakayetoka katika viuno vyako mwenyewe ndiye atakayekuwa mrithi wako.” Akamtoa nje na kusema, “Tazama juu kuelekea mbinguni na uhesabu nyota, kama hakika utaweza kuzihesabu.” Ndipo akamwambia, “Hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa.” Abramu akamwamini BWANA, naye kwake hili likahesabiwa kuwa haki.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mwanzo 15:1-6