Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 6:14-30

Kutoka 6:14-30 NEN

Hawa walikuwa wakuu wa jamaa zao: Wana wa Reubeni mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Israeli walikuwa Hanoki, Palu, Hesroni na Karmi. Hawa walikuwa ndio koo za Reubeni. Wana wa Simeoni walikuwa Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Sohari na Shauli mwana wa mwanamke Mkanaani. Hawa walikuwa ndio koo za Simeoni. Haya ndiyo majina ya wana wa Lawi kufuatana na orodha zao: Gershoni, Kohathi na Merari. Lawi aliishi miaka 137. Wana wa Gershoni kwa koo, walikuwa Libni na Shimei. Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli. Kohathi aliishi miaka 133. Wana wa Merari walikuwa Mahli na Mushi. Hizi ndizo zilizokuwa koo za Lawi kufuatana na orodha zao. Amramu akamwoa Yokebedi, shangazi yake, ambaye alimzalia Aroni na Mose. Amramu aliishi miaka 137. Wana wa Ishari walikuwa Kora, Nefegi na Zikri. Wana wa Uzieli walikuwa Mishaeli, Elisafani na Sithri. Aroni akamwoa Elisheba binti wa Aminadabu ndugu yake Nashoni, naye akamzalia Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari. Wana wa Kora walikuwa Asiri, Elikana na Abiasafu. Hawa walikuwa ndio koo za Kora. Eleazari mwana wa Aroni akamwoa mmoja wa binti za Putieli, naye akamzalia Finehasi. Hawa walikuwa ndio wakuu wa jamaa za Walawi, ukoo kwa ukoo. Hawa walikuwa Aroni na Mose wale wale ambao BWANA aliwaambia, “Watoeni Waisraeli katika nchi ya Misri kwa vikosi vyao.” Ndio hao hao waliozungumza na Farao mfalme wa Misri kuhusu kuwatoa Waisraeli Misri. Ilikuwa ni huyo Mose na huyo Aroni. BWANA aliponena na Mose huko Misri, akamwambia, “Mimi ndimi BWANA. Mwambie Farao mfalme wa Misri kila kitu nikuambiacho.” Lakini Mose akamwambia BWANA, “Kwa kuwa mimi huzungumza kwa kigugumizi, Farao atanisikiliza mimi?”

Video for Kutoka 6:14-30

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Kutoka 6:14-30