Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kutoka 34:1-9

Kutoka 34:1-9 NEN

BWANA akamwambia Mose, “Chonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza, nami nitaandika juu yake maneno yale yaliyokuwa kwenye vile vibao vya kwanza, ulivyovivunja. Uwe tayari asubuhi, kisha upande juu ya Mlima Sinai. Uje mbele zangu kukutana nami huko juu ya mlima. Mtu yeyote asije pamoja nawe, wala asionekane mtu popote juu ya mlima, wala kondoo na mbuzi au ngʼombe wasilishe karibu mbele ya huo mlima.” Kwa hiyo Mose akachonga vibao viwili vya mawe kama vile vya kwanza, naye akapanda juu ya Mlima Sinai asubuhi na mapema, kama BWANA alivyokuwa amemwagiza, akachukua vile vibao viwili vya mawe mikononi mwake. Kisha BWANA akashuka katika wingu akasimama pamoja naye huko, akalitangaza jina lake, BWANA. BWANA akapita mbele ya Mose, akitangaza, “BWANA, BWANA, Mungu mwenye huruma na neema, asiye mwepesi wa hasira, mwingi wa upendo na uaminifu, akidumisha upendo kwa maelfu, pia akisamehe uovu, uasi na dhambi. Lakini haachi kuadhibu mwenye hatia; huwaadhibu watoto na watoto wao kwa ajili ya dhambi ya baba zao hata katika kizazi cha tatu na cha nne.” Mara Mose akasujudu na kuabudu. Mose akasema, “Ee BWANA, kama nimepata kibali mbele zako, basi BWANA uende pamoja nasi. Ingawa watu hawa ni wenye shingo ngumu, samehe uovu wetu na dhambi yetu, tuchukue kuwa urithi wako.”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Kutoka 34:1-9