Waefeso 4:17-24
Waefeso 4:17-24 NEN
Hivyo nawaambia hivi, nami nasisitiza katika Bwana kwamba, msiishi tena kama watu wa Mataifa wanavyoishi, katika ubatili wa mawazo yao. Watu hao akili zao zimetiwa giza na wametengwa mbali na uzima wa Mungu kwa sababu ya ujinga wao kutokana na ugumu wa mioyo yao. Wakiisha kufa ganzi, wamejitia katika mambo ya ufisadi na kujiingiza katika kila aina ya uchafu, wakiendelea kutamani zaidi. Lakini ninyi, hivyo sivyo mlivyojifunza Kristo. Kama hivyo ndivyo ilivyo, ninyi mmemsikia, tena mmefundishwa naye, vile kweli ilivyo katika Yesu. Mlifundishwa kuuvua mwenendo wenu wa zamani, utu wenu wa kale, ulioharibiwa na tamaa zake za udanganyifu, ili mfanywe upya katika roho ya nia zenu, na mkajivike utu mpya, ulioumbwa sawasawa na mfano wa Mungu katika haki ya kweli na utakatifu.



