Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumbukumbu 5:6-21

Kumbukumbu 5:6-21 NEN

“Mimi ndimi BWANA Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa. “Usiwe na miungu mingine ila mimi. Usijitengenezee sanamu katika umbo la kitu chochote kilicho juu mbinguni au duniani chini au ndani ya maji. Usivisujudie wala kuviabudu; kwa kuwa Mimi, BWANA Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, ninayewaadhibu watoto kwa ajili ya dhambi za baba zao hadi kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, lakini ninaonyesha upendo kwa maelfu ya vizazi vya wale wanipendao na kuzishika amri zangu. Usilitaje bure jina la BWANA Mungu wako, kwa kuwa BWANA hataacha kumhesabia hatia yeye alitajaye jina lake bure. Adhimisha siku ya Sabato na kuiweka takatifu, kama BWANA Mungu wako alivyokuagiza. Kwa siku sita utafanya kazi na kutenda shughuli zako zote. Lakini siku ya Saba ni Sabato kwa BWANA, Mungu wako. Siku hiyo hutafanya kazi yoyote, wewe, wala mwanao au binti yako, wala mtumishi wa kiume au mtumishi wa kike, wala ngʼombe wako, punda wako au mnyama wako yeyote, wala mgeni aliyeko malangoni mwako, ili kwamba mtumishi wako wa kiume na wa kike wapate kupumzika kama wewe. Kumbuka mlikuwa watumwa huko Misri, na BWANA Mungu wenu aliwatoa huko kwa mkono wenye nguvu na kwa mkono ulionyooshwa. Kwa hiyo BWANA Mungu wako amekuagiza kuiadhimisha siku ya Sabato. Waheshimu baba yako na mama yako, kama BWANA Mungu wako alivyokuagiza, ili siku zako zipate kuwa nyingi na kufanikiwa katika nchi BWANA Mungu wako anayokupa. Usiue. Usizini. Usiibe. Usimshuhudie jirani yako uongo. Usitamani mke wa jirani yako. Usitamani nyumba ya jirani yako au shamba lake, mtumishi wake wa kiume au wa kike, ngʼombe au punda wake, wala kitu chochote cha jirani yako.”