Kumbukumbu 28:7-9
Kumbukumbu 28:7-9 NENO
Mwenyezi Mungu atasababisha adui wainukao dhidi yako kushindwa mbele yako. Watakujia kwa njia moja lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. Mwenyezi Mungu ataagiza baraka juu ya ghala zako na juu ya kila kitu utakachogusa kwa mkono wako. Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakubariki katika nchi anayokupa. Mwenyezi Mungu atakufanya kuwa taifa lake takatifu, kama alivyokuahidi kwa kiapo, ukishika maagizo ya Mwenyezi Mungu, Mungu wako, na kwenda katika njia zake.