Kumbukumbu 28:7-8
Kumbukumbu 28:7-8 NEN
BWANA atasababisha adui wainukao dhidi yako kushindwa mbele yako. Watakujia kwa njia moja lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba. BWANA ataagiza baraka juu ya ghala zako na juu ya kila kitu utakachogusa kwa mkono wako. BWANA Mungu wako atakubariki katika nchi anayokupa.