Kumbukumbu 18:15-19
Kumbukumbu 18:15-19 NEN
BWANA Mungu wenu atawainulia nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu wenyewe. Msikilizeni yeye. Kwa kuwa hivi ndivyo mlivyomwomba BWANA Mungu wenu kule Horebu siku ile ya kusanyiko, wakati mliposema, “Na tusiisikie sauti ya BWANA Mungu wetu, wala kuuona moto huu mkubwa tena, ama sivyo tutakufa.” BWANA akaniambia: “Wanachosema ni vyema. Nitawainulia nabii kama wewe kutoka miongoni mwa ndugu zao; nitaweka maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia kila kitu nitakachomwamuru. Kama mtu yeyote hatasikiliza maneno yangu ambayo huyo nabii atayasema kwa Jina langu, mimi mwenyewe nitamwajibisha.