Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Kumbukumbu 11:8-14

Kumbukumbu 11:8-14 NENO

Kwa hiyo fuateni maagizo yote ninayowapa leo, ili mpate kuwa na nguvu za kuingia na kuiteka nchi ambayo mnavuka Yordani kuimiliki, ili mpate kuishi siku nyingi katika nchi ambayo Mwenyezi Mungu aliapa kuwapa baba zenu na wazao wao, nchi inayotiririka maziwa na asali. Nchi mnayoiingia kuimiliki haifanani na nchi ya Misri mlikotoka, ambako mlipanda mbegu zenu na kunyunyizia maji kwa miguu kama bustani ya mboga. Lakini nchi mnayovuka Yordani kuimiliki ni nchi ya milima na mabonde inayokunywa maji ya mvua ya mbinguni. Ni nchi ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anaitunza; macho ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, yanaitazama daima kutoka mwanzo wa mwaka hadi mwisho wa mwaka. Hivyo mkiyatii maagizo yangu ninayowapa leo kwa uaminifu, yaani kwa kumpenda Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, na kumtumikia kwa moyo wako wote na kwa roho yenu yote, ndipo atawanyeshea mvua katika nchi yenu kwa majira yake, mvua ya masika na ya vuli, ili mpate kuvuna nafaka zenu, divai mpya na mafuta.