Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Amosi 7:1-9

Amosi 7:1-9 NENO

Hili ndilo alilonionesha Bwana Mungu Mwenyezi katika maono: Alikuwa anaandaa makundi ya nzige baada ya kuvunwa fungu la mfalme na wakati ule tu mimea ya pili ilipokuwa ikichipua. Wakati nzige walikuwa wamekula mimea yote ya nchi, nililia kwa sauti kuu, “Bwana Mungu Mwenyezi, samehe! Je, Yakobo atawezaje kuendelea kuishi? Yeye ni mdogo sana!” Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akaghairi. Kisha Mwenyezi Mungu akasema, “Hili halitatokea.” Hili ndilo Bwana Mungu Mwenyezi alilonionesha katika maono: Bwana Mungu Mwenyezi alikuwa akiita hukumu ya moto; nao ulikausha vilindi vikuu, ukateketeza nchi. Ndipo nikalia, “Bwana Mungu Mwenyezi, nakusihi, zuia! Je, Yakobo atawezaje kuendelea kuishi? Yeye ni mdogo sana!” Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akaghairi. Bwana Mungu Mwenyezi akasema, “Hili nalo halitatokea.” Hili ndilo alilonionesha katika maono: Bwana alikuwa amesimama karibu na ukuta ambao ulikuwa umejengwa kwa timazi, akiwa na uzi wa timazi mkononi mwake. Naye Mwenyezi Mungu akaniuliza, “Je, Amosi unaona nini?” Nikamjibu, “Uzi wa timazi.” Kisha Bwana akasema, “Tazama, ninaweka uzi wa timazi miongoni mwa watu wangu Israeli; sitawahurumia tena. “Mahali pa Isaka pa juu pa kuabudia pataangamizwa, na mahali patakatifu pa Israeli pa kuabudia pataharibiwa; kwa upanga wangu nitainuka dhidi ya nyumba ya Yeroboamu.”