Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Amosi 3:1-8

Amosi 3:1-8 NENO

Sikilizeni neno hili alilosema Mwenyezi Mungu dhidi yenu, enyi watu wa Israeli, dhidi ya jamaa nzima niliowapandisha toka Misri: “Ni ninyi tu niliowachagua kati ya jamaa zote za dunia; kwa hiyo nitawaadhibu kwa ajili ya dhambi zenu zote.” Je, watu wawili hutembea pamoja wasipokubaliana kufanya hivyo? Je, simba hunguruma katika kichaka wakati hana mawindo? Aweza kuvuma katika pango wakati ambao hajakamata chochote? Je, ndege aweza kuanguka kwenye mtego ulio ardhini ambapo hajategewa chambo? Je, mtego unaweza kufyatuka toka ardhini wakati hakuna chochote cha kunasa? Je, tarumbeta inapopigwa mjini kujulisha hatari, watu hawatetemeki? Mji unapopatwa na maafa, je, si Mwenyezi Mungu amesababisha? Hakika Bwana Mungu Mwenyezi hatafanya neno lolote bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake. Simba amenguruma: je, ni nani ambaye hataogopa? Bwana Mungu Mwenyezi ametamka: je, ni nani awezaye kukosa kutoa unabii?