Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Nyakati 7:1-4

2 Nyakati 7:1-4 NEN

Baada ya Solomoni kumaliza kuomba, moto ukashuka kutoka mbinguni na kuteketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu, nao utukufu wa BWANA ukalijaza Hekalu. Makuhani hawakuweza kuingia ndani ya Hekalu la BWANA kwa sababu utukufu wa BWANA ulilijaza. Waisraeli wote walipoona moto ukishuka na utukufu wa BWANA ukiwa juu ya Hekalu, wakapiga magoti sakafuni wakasujudu nyuso zao mpaka chini, nao wakamwabudu na kumshukuru BWANA wakisema, “Yeye ni mwema; upendo wake unadumu milele.” Ndipo mfalme na watu wote wakatoa dhabihu mbele za BWANA Mungu.