Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Samweli 24:4-8

1 Samweli 24:4-8 NEN

Watu wa Daudi wakasema, “Hii ndiyo siku aliyonena BWANA akikuambia, ‘Nitamtia adui yako mikononi mwako ili wewe umtendee utakavyo.’ ” Basi Daudi akanyemelea bila kuonekana na kukata upindo wa joho la Sauli. Baada ya hilo, dhamiri ya Daudi ikataabika kwa kukata upindo wa joho la Sauli. Akawaambia watu wake, “BWANA na apishie mbali nisije nikafanya jambo kama hilo kwa bwana wangu, yeye ambaye ni mpakwa mafuta wa BWANA, au kuinua mkono wangu dhidi yake; kwani yeye ni mpakwa mafuta wa BWANA.” Kwa maneno haya Daudi akawaonya watu wake na hakuwaruhusu wamshambulie Sauli. Naye Sauli akaondoka pangoni na kwenda zake. Ndipo Daudi naye akatoka pangoni na kumwita Sauli akisema, “Mfalme, bwana wangu!” Sauli alipotazama nyuma, Daudi akainama na kusujudu uso wake mpaka nchi.