1 Samweli 15:22-23
1 Samweli 15:22-23 NENO
Lakini Samweli akajibu: “Je, Mwenyezi Mungu anafurahia sadaka za kuteketezwa na dhabihu kama vile kuitii sauti ya Mwenyezi Mungu? Kutii ni bora kuliko dhabihu, nako kusikia ni bora kuliko mafuta ya kondoo dume. Kwa maana kuasi ni kama dhambi ya uaguzi, nao ukaidi ni kama uovu wa kuabudu sanamu. Kwa sababu umelikataa neno la Mwenyezi Mungu, naye amekukataa wewe kuendelea kuwa mfalme.”