1 Wafalme 11:9-13
1 Wafalme 11:9-13 NENO
Mwenyezi Mungu akamkasirikia Sulemani kwa sababu moyo wake uligeuka mbali na Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, aliyekuwa amemtokea mara mbili. Ingawa alikuwa amemkataza Sulemani kufuata miungu mingine, Sulemani hakutii amri ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akamwambia Sulemani, “Kwa kuwa huu ndio msimamo wako, na hukushika agano langu na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitakunyang’anya ufalme na kumpa mmoja wa walio chini yako. Hata hivyo, kwa ajili ya Daudi baba yako, sitafanya jambo hili wakati wa uhai wako. Nitaurarua kutoka mikononi mwa mwanao. Lakini pia sitaurarua ufalme wote kutoka kwake, bali nitampa kabila moja kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu na kwa ajili ya Yerusalemu, ambao nimeuchagua.”