1 Wakorintho 12:1-3
1 Wakorintho 12:1-3 NENO
Basi ndugu zangu, kuhusu karama za rohoni, sitaki mkose kufahamu. Mnajua kwamba mlipokuwa watu wasiomjua Mungu, kwa njia moja au nyingine mlishawishika na kupotoshwa mkielekezwa kwa sanamu zisizonena. Kwa hiyo nawaambieni ya kuwa hakuna mtu anayeongozwa na Roho Mtakatifu wa Mungu anayeweza kusema, “Isa na alaaniwe.” Pia hakuna mtu awezaye kusema, “Isa ni Bwana,” isipokuwa ameongozwa na Roho wa Mungu.