Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Wakorintho 11:27-34

1 Wakorintho 11:27-34 NENO

Kwa hiyo, mtu yeyote alaye mkate huo au kukinywea kikombe hicho cha Bwana Isa isivyostahili, atakuwa na hatia ya dhambi juu ya mwili na damu ya Bwana Isa. Inampasa mtu ajichunguze mwenyewe, kabla ya kula mkate na kukinywea kikombe. Kwa maana mtu yeyote alaye na kunywa pasipo kuutambua mwili wa Bwana Isa, hula na kunywa hukumu juu yake mwenyewe. Hii ndiyo sababu wengi miongoni mwenu ni wagonjwa na dhaifu na wengine wenu hata wamekufa. Lakini kama tungejichunguza wenyewe tusingehukumiwa. Tunapohukumiwa na Bwana Isa, tunaadibishwa ili tusije tukahukumiwa pamoja na ulimwengu. Kwa hiyo, ndugu zangu, mkutanikapo pamoja ili kula, mngojane. Kama mtu akiwa na njaa, ale nyumbani mwake ili mkutanapo pamoja msije mkahukumiwa. Nami nitakapokuja nitawapa maelekezo zaidi.