1 Nyakati 12:17-23
1 Nyakati 12:17-23 NENO
Daudi akatoka nje kuwalaki na akawaambia, “Kama mmekuja kwangu kwa amani, kunisaidia, mimi niko tayari kuwaruhusu ninyi kuungana nami. Lakini kama mmekuja ili kunisaliti kwa adui zangu wakati mikono yangu haina hatia, basi Mungu wa baba zetu aone na awahukumu.” Kisha Roho wa Mungu akaja juu ya Amasai, mkuu wa wale Thelathini, naye akasema: “Sisi tu watu wako, ee Daudi! Nasi tuko pamoja na wewe, ee mwana wa Yese! Amani, naam, amani iwe kwako, pia amani kwa wale walio upande wako, kwa kuwa Mungu wako atakusaidia.” Kwa hiyo Daudi akawapokea na kuwafanya viongozi wa vikosi vyake vya uvamizi. Baadhi ya watu kutoka kabila la Manase wakajiunga na Daudi alipoenda pamoja na Wafilisti kupigana na Sauli. (Daudi na watu wake hawakuwasaidia Wafilisti kwa sababu baada ya ushauri, watawala wao walimrudisha. Wakasema, “Itatugharimu vichwa vyetu kama Daudi atatuasi na kurudi kwa Sauli bwana wake.”) Daudi alipoenda Siklagi, hawa ndio wanaume wa kabila la Manase waliojiunga naye: Adna, Yozabadi, Yediaeli, Mikaeli, Yozabadi, Elihu na Silethai, viongozi wa vikosi vya watu elfu moja katika kabila la Manase. Walimsaidia Daudi dhidi ya makundi ya uvamizi, kwa kuwa wote walikuwa mashujaa hodari na walikuwa majemadari katika jeshi lake. Siku baada ya siku watu walikuja kumsaidia Daudi, hadi akawa na jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu. Hawa ndio watu waliojiandaa kwa ajili ya vita waliokuja kwa Daudi huko Hebroni ili kumtwalia ufalme kutoka kwa Sauli, kama Mwenyezi Mungu alivyokuwa amesema