Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Nyakati 11:1-9

1 Nyakati 11:1-9 NENO

Waisraeli wote walimjia Daudi kwa pamoja huko Hebroni, wakamwambia, “Sisi ni mwili wako na damu yako. Zamani, wakati Sauli alikuwa mfalme, wewe ndiwe uliyeiongoza Israeli vitani, naye Mwenyezi Mungu, Mungu wako, alikuambia, ‘Wewe utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala wao.’ ” Wazee wote wa Israeli walipokuwa wamewasili kwa Mfalme Daudi huko Hebroni, alifanya mapatano nao huko Hebroni mbele za Mwenyezi Mungu, nao wakampaka Daudi mafuta awe mfalme wa Israeli, sawasawa na neno la Mwenyezi Mungu aliloahidi kupitia kwa Samweli. Daudi na Waisraeli wote wakaenda Yerusalemu (ndio Yebusi). Nao Wayebusi walioishi humo wakamwambia Daudi, “Wewe hutaingia humu.” Hata hivyo, Daudi akaiteka ngome ya Sayuni, Mji wa Daudi. Daudi alikuwa amesema, “Yeyote atakayeongoza mashambulizi dhidi ya Wayebusi atakuwa jemadari mkuu.” Yoabu mwana wa Seruya akawa wa kwanza kukwea, naye akawa mkuu. Daudi akafanya makao yake kwenye ngome, hivyo ukaitwa Mji wa Daudi. Akajenga mji pande zote, kuanzia Milo hadi kwenye ukuta kuzunguka; wakati huo huo Yoabu akajenga sehemu zingine zilizobaki za Yerusalemu. Daudi akazidi kuwa na nguvu zaidi na zaidi, kwa sababu Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni alikuwa pamoja naye.