1
Kumbukumbu la Sheria 7:9
Biblia Habari Njema
Basi, jueni kwamba Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, ndiye Mungu; ni Mungu mwaminifu, anayeshika agano lake na huwaonesha fadhili kwa vizazi vingi vya wale wanaoshika amri zake.
Linganisha
Chunguza Kumbukumbu la Sheria 7:9
2
Kumbukumbu la Sheria 7:6
Fanyeni hivyo kwa kuwa nyinyi mmewekwa wakfu kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Kati ya watu wote ulimwenguni aliwachagua nyinyi ili muwe taifa lake mwenyewe.
Chunguza Kumbukumbu la Sheria 7:6
3
Kumbukumbu la Sheria 7:8
Lakini ni kwa sababu Mwenyezi-Mungu anawapenda na anashika kiapo alichowaapia babu zenu, ndiyo maana aliwaokoeni kwa mkono wake wenye nguvu na kuwaokoa toka utumwani, toka mikono ya Farao mfalme wa Misri.
Chunguza Kumbukumbu la Sheria 7:8
4
Kumbukumbu la Sheria 7:7
“Mwenyezi-Mungu hakuwapenda nyinyi na kuwateua kwa kuwa nyinyi ni wengi mno kuliko watu wengine; nyinyi mlikuwa wachache kuliko mataifa mengine duniani.
Chunguza Kumbukumbu la Sheria 7:7
5
Kumbukumbu la Sheria 7:14
Mtabarikiwa kuliko watu wengine wote ulimwenguni. Miongoni mwenu hakutakuwa na mwanamume wala mwanamke tasa.
Chunguza Kumbukumbu la Sheria 7:14
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video