1
Yohana 7:38
Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Yeyote aniaminiye mimi, kama Maandiko yanavyosema, vijito vya maji ya uzima vitatiririka kutoka ndani yake.”
Linganisha
Chunguza Yohana 7:38
2
Yohana 7:37
Siku ile ya mwisho ya Sikukuu, siku ile kuu, wakati Isa akiwa amesimama huko, akapaza sauti yake akasema, “Kama mtu yeyote anaona kiu na aje kwangu anywe.
Chunguza Yohana 7:37
3
Yohana 7:39
Isa aliposema haya, alimaanisha Roho Mtakatifu wa Mungu, ambaye wote waliomwamini wangempokea. Kwa maana hadi wakati huo Roho wa Mungu alikuwa hajatolewa, kwa kuwa Isa alikuwa bado hajatukuzwa.
Chunguza Yohana 7:39
4
Yohana 7:24
Acheni kuhukumu mambo kwa jinsi mnavyoona tu, bali hukumuni kwa haki.”
Chunguza Yohana 7:24
5
Yohana 7:18
Wale wanenao kwa ajili yao wenyewe hufanya hivyo kwa kutaka utukufu wao wenyewe. Lakini yeye atafutaye utukufu wa yule aliyemtuma ni wa kweli, wala hakuna uongo ndani yake.
Chunguza Yohana 7:18
6
Yohana 7:16
Ndipo Isa akawajibu, “Mafundisho yangu si yangu mwenyewe, bali yanatoka kwake yeye aliyenituma.
Chunguza Yohana 7:16
7
Yohana 7:7
Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, lakini unanichukia mimi kwa sababu ninawashuhudia kwamba matendo yao ni maovu.
Chunguza Yohana 7:7
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video