Bassi walipokwisha kula, Yesu akamwambia Simon Petro, Simon wa Yohana, wanipenda kuliko bawa? Akamwambia, Naam, Bwana; wewe wajua ya kuwa nakupenda. Akamwambia, Lisha wana kondoo wangu. Akamwambia marra ya pili, Simon wa Yohana, wanipenda? Akamwambia, Naam, Bwana; wewe wajua ya kuwa nakupenda. Akamwambia, Chunga kondoo zangu. Akamwambia marra ya tatu, Simon wa Yohana, Wanipenda mimi? Petro akahuzunika kwa kuwa alimwambia marra ya tatu, Wanipenda mimi? Akamwambia, Bwana, wewe unajua yote; unajua ya kuwa nakupenda. Yesu amwambia, Lisha kondoo zangu.