1
Yohana 16:33
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
“Nimewaambia mambo haya ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki. Lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu.”
Linganisha
Chunguza Yohana 16:33
2
Yohana 16:13
Atakapokuja huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie katika kweli yote. Yeye hatanena kwa ajili yake mwenyewe, bali atanena yale yote atakayosikia, naye atawaonesha mambo yajayo.
Chunguza Yohana 16:13
3
Yohana 16:24
Hadi sasa hamjaomba jambo lolote kwa Jina langu. Ombeni nanyi mtapewa, ili furaha yenu ipate kuwa kamili.
Chunguza Yohana 16:24
4
Yohana 16:7-8
Lakini nawaambia kweli, yafaa mimi niondoke, kwa kuwa nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; lakini nikienda nitamtuma kwenu. Naye atakapokuja, atauthibitishia ulimwengu kuhusu dhambi, haki na hukumu.
Chunguza Yohana 16:7-8
5
Yohana 16:22-23
Hivyo ninyi mna maumivu sasa, lakini nitawaona tena, nayo mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye. Katika siku hiyo hamtaniuliza neno lolote. Amin, amin nawaambia, mkimwomba Baba jambo lolote kwa jina langu, yeye atawapa.
Chunguza Yohana 16:22-23
6
Yohana 16:20
Amin, amin nawaambia, ninyi mtalia na kuomboleza, lakini ulimwengu utafurahi. Ninyi mtahuzunika, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha.
Chunguza Yohana 16:20
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video