1
Marko 8:35
Swahili Revised Union Version
Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya Injili, huyu ataisalimisha.
Linganisha
Chunguza Marko 8:35
2
Marko 8:36
Kwa kuwa itamfaidi mtu nini kuupata ulimwengu wote, akiipoteza nafsi yake?
Chunguza Marko 8:36
3
Marko 8:34
Akawaita mkutano pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, Mtu yeyote akitaka kunifuata na ajikane mwenyewe, ajitwike na msalaba wake, anifuate.
Chunguza Marko 8:34
4
Marko 8:37-38
Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake? Maana kila mtu atakayenionea haya mimi, na maneno yangu, katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.
Chunguza Marko 8:37-38
5
Marko 8:29
Naye akawauliza, Na ninyi mnasema ya kuwa mimi ni nani? Petro akamjibu, akamwambia, Wewe ndiwe Kristo.
Chunguza Marko 8:29
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video