1
Marko 7:21-23
Swahili Revised Union Version
Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.
Linganisha
Chunguza Marko 7:21-23
2
Marko 7:15
Hakuna kitu kilicho nje ya mtu ambacho kikimwingia chaweza kumtia unajisi, bali vile vimtokavyo, ndivyo vimtiavyo unajisi yule mtu. [
Chunguza Marko 7:15
3
Marko 7:6
Akawaambia, Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa, Watu hawa huniheshimu kwa midomo Ila mioyo yao iko mbali nami
Chunguza Marko 7:6
4
Marko 7:7
Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu
Chunguza Marko 7:7
5
Marko 7:8
Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu.
Chunguza Marko 7:8
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video