1
Mathayo 27:46
Swahili Revised Union Version
Na kama saa tisa, Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu akisema, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Yaani, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?
Linganisha
Chunguza Mathayo 27:46
2
Mathayo 27:51-52
Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hadi chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka; makaburi yakafunuka; ikainuka miili mingi ya watakatifu waliolala
Chunguza Mathayo 27:51-52
3
Mathayo 27:50
Naye Yesu akiisha kupaza sauti tena kwa nguvu, akaitoa roho yake.
Chunguza Mathayo 27:50
4
Mathayo 27:54
Basi yule afisa, na hao waliokuwa pamoja naye wakimlinda Yesu, walipoliona tetemeko la ardhi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakisema, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.
Chunguza Mathayo 27:54
5
Mathayo 27:45
Basi tangu saa sita palikuwa na giza juu ya nchi yote hadi saa tisa.
Chunguza Mathayo 27:45
6
Mathayo 27:22-23
Pilato akawaambia, Basi, nimtendeje Yesu aitwaye Kristo? Wakasema wote, Asulubiwe. Akasema, Kwa nini? Ni ubaya gani alioutenda? Wakazidi sana kupiga kelele, wakisema, Na asulubiwe.
Chunguza Mathayo 27:22-23
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video