1
Wafilipi 3:13-14
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Ndugu zangu, sijihesabu kuwa nimekwisha kushika. Lakini ninafanya jambo moja: Ninasahau mambo yale yaliyopita, nakaza mwendo kufikia yale yaliyo mbele. Nakaza mwendo nifikie ile alama ya ushindi iliyowekwa ili nipate tuzo ya mwito mkuu wa Mungu ambao nimeitiwa huko juu mbinguni katika Al-Masihi Isa.
Linganisha
Chunguza Wafilipi 3:13-14
2
Wafilipi 3:10-11
Nataka nimjue Al-Masihi na uweza wa kufufuka kwake na ushirika wa mateso yake, ili nifanane naye katika mauti yake, ili kwa njia yoyote niweze kufikia ufufuo wa wafu.
Chunguza Wafilipi 3:10-11
3
Wafilipi 3:8
Zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara tupu nikiyalinganisha na faida kubwa ipitayo kiasi cha kumjua Al-Masihi Isa Bwana wangu, ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote, nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nimpate Al-Masihi.
Chunguza Wafilipi 3:8
4
Wafilipi 3:7
Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, sasa nayahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Al-Masihi.
Chunguza Wafilipi 3:7
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video