1
Marko 7:21-23
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Kwa maana kutoka ndani ya moyo wa mtu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, matukano, kiburi na upumbavu. Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu, nayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi.”
Linganisha
Chunguza Marko 7:21-23
2
Marko 7:15
Hakuna kitu kinachomwingia mtu kimtiacho unajisi, lakini kile kimtokacho ndicho kimtiacho unajisi. [
Chunguza Marko 7:15
3
Marko 7:6
Isa akawajibu, “Nabii Isaya alisema ukweli alipotabiri juu yenu, ninyi wanafiki. Kama ilivyoandikwa: “ ‘Watu hawa huniheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami.
Chunguza Marko 7:6
4
Marko 7:7
Huniabudu bure, nayo mafundisho yao ni maagizo ya wanadamu tu.’
Chunguza Marko 7:7
5
Marko 7:8
Ninyi mmeziacha amri za Mungu na kushika desturi za watu.”
Chunguza Marko 7:8
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video