Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto wa kiume na utamwita jina Isa. Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu Sana. Mwenyezi Mungu atampa kiti cha utawala cha Daudi baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho.”