Kwa maana hili ndilo asemalo Aliye juu,
yeye aliyeinuliwa sana,
yeye aishiye milele,
ambaye jina lake ni Mtakatifu:
“Ninaishi mahali palipoinuka
na patakatifu,
lakini pia pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu,
na mwenye roho ya unyenyekevu,
ili kuzihuisha roho za wanyenyekevu
na kuihuisha mioyo yao waliotubu.
Sitaendelea kulaumu milele,
wala sitakasirika siku zote,
kwa kuwa roho ya mwanadamu
ingezimia mbele zangu:
yaani pumzi ya mwanadamu niliyemuumba.