Lakini sasa uwe imara, ee Zerubabeli,’ asema Mwenyezi Mungu. ‘Kuwa imara, ee kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehosadaki. Mwe imara, enyi watu wote wa nchi,’ asema Mwenyezi Mungu, ‘na mfanye kazi. Kwa kuwa mimi nipo pamoja nanyi,’ asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.