“ ‘Hili ndilo asemalo Bwana Mungu Mwenyezi: Mimi mwenyewe nitachukua chipukizi kutoka kilele cha juu sana cha mwerezi na kukipanda, nitavunja kitawi kichanga kutoka matawi yake ya juu kabisa na kukipanda juu ya mlima mrefu ulioinuka sana. Katika vilele vya mlima mrefu wa Israeli nitakipanda, kitatoa matawi na kuzaa matunda na kuwa mwerezi mzuri sana. Ndege wa kila aina watajenga viota vyao ndani yake, nao watapata makazi katika kivuli cha matawi yake.