1
Kumbukumbu 4:29
Neno: Bibilia Takatifu
Lakini kama mtamtafuta BWANA Mungu wenu, mtampata; kama mtamtafuta kwa moyo wenu wote na kwa roho yote.
Linganisha
Chunguza Kumbukumbu 4:29
2
Kumbukumbu 4:31
Kwa maana BWANA Mungu wenu ni Mungu mwenye huruma, hatawaacha au kuwaangamiza wala kusahau Agano alilofanya na baba zenu, alilowathibitishia kwa kiapo.
Chunguza Kumbukumbu 4:31
3
Kumbukumbu 4:24
Kwa kuwa BWANA Mungu wenu ni moto ulao, Mungu mwenye wivu.
Chunguza Kumbukumbu 4:24
4
Kumbukumbu 4:9
Mwe waangalifu, na makini ili msije mkasahau mambo ambayo mliyaona kwa macho yenu, wala kuyaacha yaondoke moyoni mwenu siku zote za uhai wenu. Mwafundishe hayo watoto wenu na watoto wao baada yao.
Chunguza Kumbukumbu 4:9
5
Kumbukumbu 4:39
Kubalini na mweke moyoni leo kuwa BWANA ndiye Mungu mbinguni juu na duniani chini. Hakuna mwingine.
Chunguza Kumbukumbu 4:39
6
Kumbukumbu 4:7
Ni taifa gani jingine lililo kubwa kiasi cha kuwa na miungu yao iliyo karibu nao kama BWANA Mungu wetu alivyo karibu nasi wakati wowote tunapomwomba?
Chunguza Kumbukumbu 4:7
7
Kumbukumbu 4:30
Wakati mnapokuwa katika dhiki, nayo mambo haya yote yamewatokea siku hizo, ndipo mtamrudia BWANA Mungu wenu na kumtii.
Chunguza Kumbukumbu 4:30
8
Kumbukumbu 4:2
Usiongeze wala usipunguze chochote ninachowaamuru ninyi, ila myashike maagizo ya BWANA Mungu wenu ambayo nawapa.
Chunguza Kumbukumbu 4:2
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video