Mkimrudia Mwenyezi Mungu, ndipo wale ndugu zenu waliotekwa pamoja na watoto wenu watakapoonewa huruma na wale waliowateka na kuwaachia warudi katika nchi hii, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, ni mwenye neema na huruma, hatageuzia uso wake mbali nanyi kama mkimrudia yeye.”