1
1 Petro 3:15-16
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Bali mtukuzeni Al-Masihi kama Bwana mioyoni mwenu. Siku zote mwe tayari kumjibu mtu yeyote atakayewauliza kuhusu sababu ya tumaini lililo ndani yenu. Lakini fanyeni hivyo kwa upole na kwa heshima, mkizitunza dhamiri zenu ziwe safi, ili wale wasemao mabaya dhidi ya mwenendo wenu mzuri katika Al-Masihi waaibike kwa ajili ya masingizio yao.
Linganisha
Chunguza 1 Petro 3:15-16
2
1 Petro 3:12
Kwa maana macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake yako makini kusikiliza maombi yao. Bali uso wa Mwenyezi Mungu uko kinyume na watendao maovu.”
Chunguza 1 Petro 3:12
3
1 Petro 3:3-4
Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje tu, kama vile kusuka nywele, kuvalia vitu vilivyofanyizwa kwa dhahabu na kwa mavazi. Badala yake, kujipamba kwenu kuwe katika utu wenu wa moyoni, yaani uzuri usioharibika wa roho ya upole na utulivu, ambayo ni ya thamani sana machoni pa Mungu.
Chunguza 1 Petro 3:3-4
4
1 Petro 3:10-11
Kwa maana, “Yeyote apendaye uzima na kuona siku njema, basi auzuie ulimi wake usinene mabaya, na midomo yake isiseme hila. Mtu huyo lazima aache uovu, akatende mema; lazima aitafute amani na kuifuatilia sana.
Chunguza 1 Petro 3:10-11
5
1 Petro 3:8-9
Hatimaye, ninyi nyote kuweni na nia moja, wenye kuhurumiana, mkipendana kama ndugu, mkijaliana, na wanyenyekevu. Msilipe ovu kwa ovu, au jeuri kwa jeuri, bali barikini, kwa maana hili ndilo mliloitiwa ili mpate kurithi baraka.
Chunguza 1 Petro 3:8-9
6
1 Petro 3:13
Basi, ni nani atakayewadhuru mkiwa wenye juhudi katika kutenda mema?
Chunguza 1 Petro 3:13
7
1 Petro 3:11
Mtu huyo lazima aache uovu, akatende mema; lazima aitafute amani na kuifuatilia sana.
Chunguza 1 Petro 3:11
8
1 Petro 3:17
Kwa maana ni afadhali kupata mateso kwa ajili ya kutenda mema, ikiwa ni mapenzi ya Mungu, kuliko kuteseka kwa kutenda maovu.
Chunguza 1 Petro 3:17
Nyumbani
Bibilia
Mipango
Video