Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zab 30:5

Acha! Usiwe Na Wasiwasi Zaidi
Siku 7
Je! unajua Yesu anasema nini kuhusu wasiwasi wetu? Acha. Ndiyo, anatuambia tuiache. Wasiwasi ni moja ya dalili kuu kwamba imani yetu imetikisika na imani yetu iko chini. Wakati wewe au mimi tunakuwa na wasiwasi, tunakosa kuweka imani ifaayo juu ya udhibiti mkuu wa Mungu. Bado sote, bado tunafanya hivyo, sivyo? Ndiyo maana Tony Evans ameweka pamoja mpango wa kusoma wa siku 7 ili kukusaidia WEWE kushinda wasiwasi. Unaweza kuvunja mzunguko na kubadilishana wasiwasi kwa amani.

Upendo wa Kweli ni nini?
Siku 12
Kila mtu anataka kujua upendo ni kitu gani. Lakini watu wachache huangalia ni nini Biblia inasema kuhusu upendo. Upendo ni mada moja muhimu ya Maandiko na pia wema muhimu zaidi katika maisha ya Kikristo. Mpango huu kutoka Huduma za Thistlebend unashughulikia maana ya kibiblia ya upendo na jinsi ya kuboresha kumpenda Mungu na kuwapenda wengine.

Oswald Chambers: Furaha- Nguvu katika Bwana
Siku 30
Gundua hekima ya Oswald Chambers, mwandishi wa "My Utmost for His Highest", katika mkusanyiko huu wa hazina ambao unatoa ufahamu kuhusu furaha. Kila somo lina dondoo kutoka Chambers na maswali ya kutafakari kibinafsi. Akitumia hekima sahili na dhahiri kutoka Biblia kukupa motisha na changamoto, utaanza kutamani kuwasiliana zaidi na Mungu.

Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023
Siku 30
Soma Biblia Kila Siku /Septemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa septemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Warumi na Methali. Karibu kujiunga na mpango huu