Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mt 28:19
MUNGU + MALENGO: Jinsi Ya Kuweka Malengo Kama Mkristo
Siku 5
Ni vyema kuweka malengo kama Mkristo. Unajuaje kama lengo lako ni kutoka kwa Mungu au kwako mwenyewe?. Na malengo ya kikristo yanaonekanaje? Katika siku 5 za mpango huu wa kusoma, utajifunza katika neno na kupata ufasaha na muelekeo juu ya kupanga mipango inayosukumwa na neema!
Nuru
5 Siku
Yesu anatueleza katika Agizo Kuu kwamba tunapaswa kwenda na kufanya wanafunzi wa mataifa yote. Lakini mfuasi wa Yesu hufanya wanafunzi vipi? Mpango huu wa usomaji unatoa mfumo wa kibiblia wa jinsi waumini wanavyofundisha wengine kutii kila kitu Yesu alichoamuru, katika kutembea kwao binafsi na Yeye na pamoja na jamii ya waumini.
Uamuzi Mkubwa Zaidi wa Maisha Yako!
Siku 6
Maamuzi mengi katika maisha huwa na athari fulani. Hata hivyo, ni uamuzi mmoja tu ndio muhimu zaidi. Kama unatafuta maelekezo rahisi ya kukuwezesha kuelewa kwa undani juu ya uamuzi huu wa ajabu – zawadi ya bure ya wokovu ya Mungu - basi anzia hapa. Imechukuliwa kutoka kitabu kiitwacho, “Nje ya Dunia Hii: Mwongozo wa Kikristo katika Kukua na Kusudi ” kilichoandikwa na David J. Swandt
Nenda Tenda Sema Toa: Uhuru wa Kujisalimisha kwa Yesu
Siku 7
Kujisalimisha kwa Yesu ni tukio kubwa maishani. Lakini uamuzi huu unamaanisha nini na tutauishi vipi kila siku? Uamuzi ni wa mambo makubwa ya maisha pekee, ama wacha Mungu kupita kiasi? Woga, makosa yaliyopita, na kutoelewa vinaweza kutuzuia. "Nenda Tenda Sema Toa" ni ahadi/sala ambayo inafunua jinsi utakavyochukua hatua zinazofuata katika safari yako ya kiroho. Pata uhuru unaotokana na kumfuata Yesu.
Hatua Sita Ya Uongozi Bora Zaidi
Siku 7
U tayari kukua kama kiongozi? Craig Groeschel anafafanua hatua sita ya kibiblia yeyote anaweza kuchukua ili kuwa kiongozi bora zaidi. Gundua nidhamu ya kuanza, ujasiri wa kuacha, mtu wa kumwezesha, mfumo wa kuumba, uhusiano wa kuanzilisha, na hatari ambayo unahitaji kuchukua.
Kwa pamoja: Kutafuta maisha pamoja
Siku 7
Unapofikia umri wa miaka 18, unaanza kuona kwamba unahitaji kupanga maisha yako. Itakuwaje usipofanya hivyo? Itakuwa kama ulipofikiria utakuwa sipo ulipo sasa? Hauko peke yako. Hebu tuangalie swali kuu la maisha yetu pamoja katika mpango huu wa Biblia wa siku 7 kwa pamoja, mafunzo ya vijana kutoka Life. Church.
Biblia i Hai
Siku 7
Tangu mwanzo wa wakati, neno la Mungu kwa uhakika limerejeza mioyo na mawazo ya watu--na Mungu hajamaliza bado. Katika mpango huu wa siku 7, hebu tusherehekee nguvu ya maandiko inayobadirisha kwa kuangalia kwa makini jinsi Mungu anavyotumia Biblia kubadili historia na maisha duniani kote.
Mzabibu
12 Siku
Moja ya maswali ya kawaida kwa watu ambao ni wapya katika kumfuata Yesu ni, “Nifanye nini sasa?” Ina maana gani kumpenda, kumtii, na kuwa sehemu ya jamii ya waumini? Mpango huu wa usomaji unatoa mfumo wa kibiblia wa jinsi ya kuunganisha uhusiano wako wa kibinafsi na Yesu na utume wa kanisa.
Hadithi ya Pasaka
Sike 16
Kusulubishwa na kufufuka kwa Yesu kumeelezwa katika injili zote nne. Likizo hii ya Pasaka, soma kuhusu jinsi Yesu alivyovumilia usaliti, mateso na kudhalilishwa msalabani kabla ya kubadilisha dunia kupitia tumaini lililotolewa kwa ufufuo wake. Video fupi yaeleza kila upande wa hadithi kwa kila siku ya mpango huu.
Soma Biblia Kila Siku 09/2024
30 Siku
Soma Biblia Kila Siku 09/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Tisa pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu