Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mt 20:26
Mwanamume Wa Kifalme
Siku 5
Katika historia yote, Mungu daima amewatafuta na kuwatumia wanaume kuendeleza ajenda ya Ufalme wake. Shetani anajua hili, ndiyo maana anataka kuwafungia na kuwahasi wanaume. Ulimwengu wetu unaendelea ukizorota kwa sababu wanaume hawapatikani popote. Ni wakati wa wanaume kusimama kidete. Katika mpango huu wa kusoma wa siku tano, Daktari Tony Evans atakupeleka kwenye safari ya kufanyika mwanamume ambaye Mungu alikuumba uwe.
Kusaka Ukuu
Siku 7
Wanaume hutamani kuwa wakuu. Sio tu kwamba tunatamani kuwa wakuu, bali pia tunatamani kutambuliwa kuwa wakuu. Lakini wanaume wengi hutatatizika wanapotaka kunufaika na uwezo wao wa kweli nao huishia kukimbizana na mambo yanayowapeleka mbali zaidi na pale wanapotaka kuwa. Gundua uanaume halisi na Tony Evans.
Mzabibu
12 Siku
Moja ya maswali ya kawaida kwa watu ambao ni wapya katika kumfuata Yesu ni, “Nifanye nini sasa?” Ina maana gani kumpenda, kumtii, na kuwa sehemu ya jamii ya waumini? Mpango huu wa usomaji unatoa mfumo wa kibiblia wa jinsi ya kuunganisha uhusiano wako wa kibinafsi na Yesu na utume wa kanisa.
Soma Biblia Kila Siku 11/2024
30 Siku
Soma Biblia Kila Siku 11/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Kumi na moja pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Mathayo na 2 Wafalme. Karibu kujiunga na mpango huu