Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Yn 14:27
Kupata Uhuru kutokana na Kufadhaika
Siku 5
Kufadhaika huwa, lakini hakufai kuyaendesha maisha yako. Kumpitia Kristo, tunaweza kuibadilisha, kuiona upya na kuitafsiri upya. Kama unapata changamoto na kufadhaika, angalia mpango huu wa Bibilia wa siku 5 ili ujifunze kupata uhuru na amani.
Uhakika katika siku za mashaka
Siku 5
Katikati ya mashaka, Mungu ni wa uhakika! Ungana na David Villa katika mpango wake mpya anapoangalia mashaka na hasi ili kufikia kitu kikubwa.
Kutafuta Amani
Siku 10
Unataka amani zaidi katika maisha yako? Unataka utulivu uwe zaidi ya matamanio yako? Unaweza kupata amani kutoka kwenye chanzo kimoja tuu--Mungu. Jiunge na Dkt. Charles Stanley anapokuonesha njia ya kubadilisha amani ya mawazo yako, akikupa nyenzo za kutatua majuto yaliyopita, kukabiliana na wasiwasi wa sasa, na kutuliza wasiwasi wa mambo yajayo.
Mpango Bora wa Kusoma
Siku 28
unajisihisi umezidiwa, kutoridhika, na kukwama maishani? Je unatamani maisha yako ya kila siku yaboreke? Neno la Mungu ni mwongozo kwa siku njema. Katika mpango huu wa siku 28, utagundua njia kutoka kuishi tu maisha mema, hadi kuishi maisha mema ambayo Mungu amekutazamia.
Oswald Chambers: Amani - Maisha kwenye Roho
Siku 30
Amani: Maisha ya Roho ni hazina ya msukumo ya nukuu kutoka kwenye kazi za Oswald Chambers, mwandishi mpendwa ulimwenguni wa ibada na mwandishi wa My Utmost for His Highest. Pata mapumziko kwa Mungu na pata uelewa zaidi wa umuhimu wa amani ya Mungu kwenye maisha yako.
Somabiblia Kila Siku 3
Siku 31
SomaBiblia Kila Siku 3 ni mpango mzuri wa kukusaidia kusoma Biblia kwa njia rahisi. Ufafanuzi wa somo la kila siku unakupa mwanga na kiu ya kuendelea kulitafakari Neno la Mungu ukiwa peke yako au pamoja na wenzako.
Soma Biblia Kila Siku/ Machi 2023
Siku 31
Soma Biblia Kila Siku/Machi 2023 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Machi pamoja na maelezo machache ya kukusaidia kuelewa zaidi neno ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wathesalonike na Yohana. Karibu kujiunga na mpango huu bure