Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Yak 1:2
Sanaa Ya Kustahimili
Siku 5
Maisha katika dunia hii yamejawa na majaribu .Yawezekana uko katikati ya moja ya majaribu hayo hivi sasa na ukiuliza, “kwa nini “? Au hata ,kuuliza “Nitaishije katika mapito haya? Kitabu cha Yakobo kina majibu! Katika mpango huu wa kusoma kwa siku tano,Chip Ingram anatuonyesha jinsi gani unaweza kuiona furaha ya Mungu katikati ya nyakati ngumu kwa kutumia ustadi kupitia Sanaa ya Kustahimili.
Kutorokea Misri
7 Siku
Muda mfupi baada ya ziara ya Wayahudi, ambao walijua kwamba Mfalme Herode alitaka kuua watoto wa eneo hilo, malaika alimtokea Yosefu katika ndoto kumwambia aende Misri na Maria na mtoto wa kijana Yesu. Swali 1: Ni nini unafikiri kinafanya watu watende kwa Yesu kama vile Herodi alitenda na kujaribu kumangamiza Yesu? Swali 2: Kama vile Mungu alivyomlinda Yusufu na jamaa yake, je, anatulinda kwa njia gani siku hizi? Swali 3: Unaweza kuelezea kuhusu wakati Mungu alikuhifadhi katika hali ngumu?
Kukombolewa kwa ndoto
Siku 7
Tunafanyaje wakati ndoto zetu zinapoonekana kuwa haziwezi kutimia? Ukiwa umeshinda matusi na hofu, pamoja na kuvunjika moyo baada ya ndoa kuvunjika, ninakabiliwa na swali mara kwa mara. Ikiwa unapitia uharibifu wa tukio au hasara, au kuchanganyikiwa baada ya kusubiri jambo kwa muda mrefu, ndoto ya Mungu kwa maisha yako bado iko hai! Rafiki ni wakati wa kuwa na ndoto tena.
Mpango Bora wa Kusoma
Siku 28
unajisihisi umezidiwa, kutoridhika, na kukwama maishani? Je unatamani maisha yako ya kila siku yaboreke? Neno la Mungu ni mwongozo kwa siku njema. Katika mpango huu wa siku 28, utagundua njia kutoka kuishi tu maisha mema, hadi kuishi maisha mema ambayo Mungu amekutazamia.
Oswald Chambers: Furaha- Nguvu katika Bwana
Siku 30
Gundua hekima ya Oswald Chambers, mwandishi wa "My Utmost for His Highest", katika mkusanyiko huu wa hazina ambao unatoa ufahamu kuhusu furaha. Kila somo lina dondoo kutoka Chambers na maswali ya kutafakari kibinafsi. Akitumia hekima sahili na dhahiri kutoka Biblia kukupa motisha na changamoto, utaanza kutamani kuwasiliana zaidi na Mungu.
Jolt ya Furaha
Siku 31
Biblia inatuambia kwamba "Katika uwepo wake kuna furaha tele" na kuwa "furaha ya Bwana ni nguvu yetu". Furaha sio hisia tu bali ni tunda la Roho na mojawapo ya silaha bora katika gala letu la kupigana na kuvunjika moyo, huzuni na kushindwa. Tumia siku 31 ukijifunza ni nini Biblia inasema kuhusu Furaha na kujiimarisha kuwa Mkristo mwenye Furaha bila wasi wasi.
Soma Biblia Kila Siku Mei/2022
Siku 31
Soma Biblia Kila Siku Mei/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Mei pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha 1 Wafalme na Yakobo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure