Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mwa 2:3
Bila Utulivu
Siku 3
"Mioyo yetu haina utulivu mpaka ipate ulivu kwako." Haijawahi kutokea kuwa wengi wetu tukakosa utulivu Agustine alielezea kwa hii sentesi maarufu. Lakini suluhisho kwa kukosa utulivu wa kweli kwetu ni nini? Huu mpango wa siku tatu utakuonesha, suluhisho kwa sehemu katika kuona vitendo vya kale vya sabato kwa lenzi tofauti ya "wewe" -- Yesu ndie mwanzo wa amani.
Kuweka Muda Wa Kupumzika
siku 5
Kupenda kazi sana na wakati wote kufanya kazi vinasifiwa sana katika ulimwengu wetu, na vinaweza kuwa ni changamoto kwa wengine. Ili kutimiza majukumu yetu na mipango yetu kwa ufanisi, lazima tujifunze kupumzika au hatutakuwa na cha kuchangia kwa tunaowapenda na kwa malengo tuliyoyaweka. Hebu tuchukue siku tano zijazo kujifunza kuhusu kupumzika na jinsi tunavyoweza kutumia tuliyojifunza maishani mwetu.
Tabia
SIku 6
Mabadiliko si rahisi, lakini si kwamba hayawezekani. Kuanza tabia chache rahisi itabadilisha jinsi unajiona leo na kukugeuza uwe mtu ambaye ungependa kuwa kesho. Mpango huu wa Biblia wa Life.Church unatazama Maandiko ili kutengeneza tabia za kila siku ambazo zitadumu.
Kutaka
Siku 7
Katika siku hizi 7 za kusoma na kujifunza, Beth Moore anatumia maswali kutoka katika Maandiko Matakatifu ili kukuongoza kwenye uhusiano wa ndani zaidi na Yeye anayekujua vizuri. Alama za uandishi zilizopotoka mwisho wa sentensi zinaonyesha udadisi, hamu au labda wasiwasi. Swali ni mwaliko toka katika hali hatarishi hadi ukaribu wa ndani zaidi. Biblia haiachi ukaribisho huo. Mara kwa mara tunaona watu wa Mungu wakimuuliza Muumbaji wao maswali. Na pia tunamwona Mungu Muumbaji akiuliza maswali kwa viumbe wake. Changamoto ni kupokea mwaliko. Jifunze kuchimba ndani ya Neno la Mungu, kujibu maswali ya Mungu, na kuleta maswali mbele Zake. Ruhusu alama za uandishi zilizopotoka ziwe ramani ya kusogeza uhusiano wako na Baba yako kuwa wa ukaribu zaidi.
Hatua Sita Ya Uongozi Bora Zaidi
Siku 7
U tayari kukua kama kiongozi? Craig Groeschel anafafanua hatua sita ya kibiblia yeyote anaweza kuchukua ili kuwa kiongozi bora zaidi. Gundua nidhamu ya kuanza, ujasiri wa kuacha, mtu wa kumwezesha, mfumo wa kuumba, uhusiano wa kuanzilisha, na hatari ambayo unahitaji kuchukua.