Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Gal 3:11
Imani
Siku 12
Je, kuona ni kuamini? Au kuamini ni kuona? Hayo ni maswali ya imani. Mpango huu unatoa masomo ya kina kuhusu imani—kutoka kwa hadithi za Agano la Kale kuhusu watu halisia ambao walionyesha imani jasiri katika matukio yasiowezekana kwa mafundisho ya Yesu juu ya somo. Kupitia kwa kusoma kwako, utatiwa moyo ili kudumisha uhusiano wako na Mungu na uwe mfuasi mwenye imani zaidi wa Yesu.
Mwaka Mpya, Rehema Mpya
SIku 15
Kwa siku 15 zifuatazo, Paul David Tripp atakukumbusha kuhusu neema ya Mungu kwako—ukweli ambao daima si wa kale. Wakati ambapo “urekebishaji wa tabia” na semi za kukutia moyo hazitoshi kukufanya uwe mtu mpya, jifunze kutumainia wema wa Mungu, kutegemea neema yake, na kuishi kwa ajili ya utukufu wake kila siku.
Soma Biblia Kila Siku Septemba 2022
Siku 30
Soma Biblia Kila Siku Septemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Septemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Wagalatia na Hagai. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure