Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Efe 5:25
Upendo na Ndoa
Siku 5
Kwa kuangazia ndoa yetu ndani ya muktadha wa Maandiko, tunampa Mungu fursa ya kufichua maarifa mapya kuhusu uhusiano wetu na kuimarisha kifungo chetu. Mpango huu unaangazia kifungu kilicholenga cha Maandiko na mawazo ya haraka kila siku ili kuanzisha majadiliano na maombi na mwenzi wako. Mpango huu wa siku tano ni ahadi ya muda mfupi ya kukusaidia kuwekeza katika uhusiano wako wa maisha. Kwa maudhui zaidi, angalia finds.life.church
Ndoa
Siku 5
Ndoa ni uhusiano wenye changamoto na tuzo na huwa tunasahau kwamba usemapo "Ndio" huo ndio mwanzo tu. Kwa bahati nzuri, Biblia ina mengi ya kusema kuhusu Ndoa kwa mtazamo wa mume na mke. Vifungu vya neno utakavyo soma katika mpango huu kila siku vimeundwa kukusaidia kuelewa muundo wa Mungu kuhusu Ndoa—na kukuza uhusiano wako na mume au mke wako.
Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022
siku 28
Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.